Wednesday, June 13, 2012

MKUTANO MKUBWA WA INJIRI KUANZA LEO

Na mwandishi wetu

MKUTANO mkubwa wa kimataifa wa injili unatarajiwa kuanza leo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam unaoongozwa na mhubiri wa kimataifa kutoka Sweeden, Mwinjilist Johaness Amritzer.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwinjilist Amritzer,  alisema kuwa mkutano huo unatarajia kuanza saa tisa alasiri ukiwa na lengo la kuonesha miujiza ya Yesu Kristo kwa wananchi wa Tanzania.

"Tunataka tuingie Tanzania kwa midundo ya kumtangaza Yesu Kristo kuwa ni bwana na mwokozi wa maisha yetu kwa sababu injili ina nguvu ya kumbadilisha kijana wa mitaani kuwa muungwana na makahaba kuwa wanawake wema," alisema Bw.Amritzer.

Alisema kuwa wageni waliotoka Marekani na Sweden ni zaidi ya 1,000 kati yao waimbaji ni 190 wakiwemo, Bi. Jenny Jensen na Bi. Julia Willkander na wachungaji kutoka katika makanisa mbalimbali ikiwemo Tanzania na Zanzibar.

Kwa upande wake Askofu wa Assembles of God kutoka mkoa wa Kilimanjaro Bw.Glorius Shoo alisema kuwa wamekusanaya wanamuziki bora kutoka hapa kwetu Tanzania.

Aliongeza kuwa mkutano huo una faida nyingi kwa Watanzania ukizingatia wataombea  amani, kufanya miujiza kwa watu wenye mahitaji mbalimbali pamoja na magonjwa sugu.

Pamoja na hayo ametoa mwito kwa Watanzania wote kujitokeza kwa wingi ili kupata ukombozi.










 

  


No comments:

Post a Comment