Wednesday, June 13, 2012

SUMATRA YANASA DALADALA 126


Na mwandishi wetu

MAMLAKA ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) inashikilia daladala zaidi ya 126 kwa kukutwa na makosa mbalimbali, yakiwemo ya kutoa lugha ya matusi, kupandisha nauli holela na mengine kutokuwa na leseni.

Taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari Dar es Salaam jana na kusainiwa na Ofisa Uhusiano wa sSUMATRA Bw. David Mziray, ilieleza kuwa katika kipindi cha Mei na Juni, 2012 mamlaka ilikamata  ya daladala zenye  makosa mbalimbali, huku wamiliki wa mabasi hayo wakitozwa faini kati ya sh 100,000 na sh 250,000.

Alisema daladala nyingi zilikamatwa kwenye mkosa ya kutokuwa na leseni, kughushi nyaraka za Serikali, kuiba njia, kutokuwa na tiketi kutovaa sale, kupakia eneo ambalo si la kitu na mengine.

Bw. Mziray alisema kutokana na hali hiyo mmiliki ambaye basi lake litabainika na makosa hayo atachukuliwa hatua za kisheria.

"Pamoja na kulipa faini hiyo mmiliki atatakiwa kusitisha mkataba na kumbadilisha dereva wa basi husika ndipo aruhusiwe kuendelea na utoaji huduma ya usafiri," alisema.


No comments:

Post a Comment