Thursday, June 21, 2012

WATAKA KATIBA YA TANGANYIKA

Na mwandishi wetu, Mara

Wananchi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara wametoa pendekezo lao la kutaka Katiba Mpya iwe ni katiba ya wananchi wa Tanganyika na si ya Muungano kwa vile Zanzibar tayari inayo katiba yake.


Pia wameiomba serikali kutoa ufafanuzi juu ya masuala muhimu
yaliyosababisha kuwepo kwa Muungano huku ikifutwa kwa serikali ya
Tanganyika iliyopata uhuru kamili kutoka kwa Waingereza mwaka 1961.

Walidai hadi sasa Zanzibar inatambulika kuwa ni nchi huru yenye mipaka
yake, serikali yake na katiba inayoiongoza wananchi wake huku
wakipendekeza nchi ya Zanzibar iruhusiwe kuwa na bendera yake katika
umoja wa mataifa.

Hayo waliyasema hivi karibuni wakati wakitoa mapendekezo yao hivi karibuni Mjini Musoma katika mdahalo wa utawala bora na uwajibikaji kupitia mchakato wa kupata Katiba Mpya ulioandaliwa na Asasi ya MDF chini ya ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society.

Walidai hakuna maana ya katiba mpya kuitwa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wakati ambapo hakuna serikali ya Tanganyika
inayodaiwa kuwa imeungana na serikali ya Zanzibar.

Wakionesha kutoridhishwa na mivutano ya Muungano waliyodai mingi
inaletwa na baadhi ya wananchi wa Zanzibar walishauri kuwa Tanganyika
pia ipewe serikali yake kamili.

Naye mwanasheria aliyekuwa mwezeshaji katika mdahalo huo Bw. Paschal
Patrober alifafanua kuwa tofauti na sababu za kiusalama mambo mengi
yaliyofanya kuwepo kwa Muungano yamebaki siri ya viongozi wakuu wa
serikali huku yakiingizwa kwa siri.




No comments:

Post a Comment