Thursday, June 21, 2012

MABALOZI WASHINDWA KUJENGA UMOJA

Mabalozi wa Afrika wanadaiwa kushindwa kujenga umoja wa nchi hizo ambapo kutokana na unyonge upo uwezekano mkubwa wa mataifa hayo kukosa nguvu

Bw. Majige Nyerere ambaye ni mtoto wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na mabalozi 11 wa mataifa ya Afrika Mabalozi hao walikwenda nyumbani kwa Mwalimu Nyerere Msasani ili kutoa msaada wa fedha dola za Marekani 6,500 kwa Mama Maria Nyerere kwa lengo la kusaidia watoto yatima mkoani Mara wanaosumbuliwa na ugonjwa wa utapiamlo


Watoto hao wanaolelewa na Mama Nyerere jukumu ambalo amelichukua kutoka kwa Mwalimu Nyerere, "Harakati za Umoja wa Afrika zimekuwa zikifanywa kwa makundi, Umoja umekuwa mgumu kuzungumzika, anayezungumzia anaonekana amechanganyikiwa"

"Historia na harakati za ukombozi hazizungumzii wala kupewa kipaumbele ikiwemo msingi wa majeshi ya Afrika" alisema Bw. Nyerere kwa uchungu

Baada ya maelezo hayo mabalozi hao walimpigia makofi ambapo Bw. Nyerere aliongeza kuwa "Kama tuna nia kweli ya kumuenzi baba yake, nchi hizo ziwajibike kuunganisha umoja huo" alisema

Awali Mama Nyerere alisema watoto yatima mkoani humo wanakabiliwa na tataizo la utapiamlo ndiyo maana amewekeza katika kilimo cha chakula ili kuwasaidia

Alisema utaratibu wa kulelea watoto wanaosumbuliwa na tatizo hilo ulianzishwa na Mwalimu Nyerere lakini baada ya kufariki ,jukumu hilo ameamua kuliendeleza

Naye Balozi wa Uganda nchini amabaye alizungumza kwa niaba ya wenzake Bw. Iblahim Mukiibi alisema kuwa nchi zao zinafahamu matatizo waliyonayo watoto yatima nchini wataendelea kuwasaidia












No comments:

Post a Comment