Friday, June 22, 2012

DIAMOND KUPAMBA MISS DAR INTER


MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nassib Adbdul ‘Diamond’ anatarajia kupamba mashindano ya kumsaka Redd's Miss Dar Intercollege 2012,yanayofanyika leo Juni 22  kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa , uliopo mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Akizungumza Dar es Salaam,Mratibu wa mashindano hayo Dina Ismail alisema mbali na Diamond, onesho hilo pia litapambwa na burudani kutoka bendi ya Skylight ambayo ipo chini ya mshiriki wa Tusker Project Fame mwaka juzi, Anneth Kushaba.

Alisema maandalizi yanakwenda vyema ambapo warembo 14, watakaosghiriki wanaendelea na mazoezi katika hoteli ya The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

“Mwaka huu tumejipanga vyema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vizuri katika fainali za Miss Tanzania,” alisema Dina.

Warembo watakaoshiriki mashindano hayo  wanatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii,  Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo Kikuu Huria (OUT ambapo taji hilo linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM.

Dina aliwataja wanyange watakaopanda jukwaani kuwa ni Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda  Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.

Mashindano hayo yamedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Redd’s, Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band, Lamada Hotel na Screen Masters.

Wengine ni Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel, Grand Villa Hotel, Spoti Kizaa zaa na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry, Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe.




No comments:

Post a Comment