Thursday, October 08, 2015

OFISI YA TAKWIMU ZINAONYESHA MFUMUKO WA BEI UMESHUKA KUFIKIA ASILIMIA 6.1


 Mkurugezi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu wa NBS, Ephraim Kwesigabo akizungumza na Waandishi wa habari leo katika ofisi za Takwimu jijini Dar es Salaam kuhusu fihirisi za bei za Taifa kwa mwezi Septemba 2015.


Wahandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo .



OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema mfumuko wa bei umeshuka hadi asilimia 6.1 kwa Septemba kutoka asilimia 6.4 kwa kipindi cha Agost 2015.

Akizungumza Dar es Salaam leo Mkurugezi wa Takwimu za Jamii na

Sensa ya Watu wa NBS, Ephraim Kwesigabo ameeleza kuwa kushuka kwa mfumuko wa bei kunachangiwa na kushuka kwa bidhaa za vyakula zinazotumiwa majumbani na kwenye migahawa pamoja na vinywaji baridi.

Amesema mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa Septemba 2015 umepungua hadi kufikia asilimia 9.6 kutoka asilimia 10.2 kwa Agosti 2015.

"Bidhaa za huduma kwa mwaka huu Septemba umepungua ikilinganishwa na kiasi cha bei kilichokuwepo Agost mwaka uliopita ambapo farihisi za bidhaa zimeongezeka hadi 159.4 na kutoka 149.93 Septemba 2014,"anaeleza.

Kwesigabo amesema mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka unapima unapima kiwango cha badiliko la kiasi cha bei za bidhaa pamoja na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

"Mfumuko wa bei ambao haujumlishi bei za vyakula  na nishati umebakia kuwa asilimia 22 kwa Septemba 2015 kama ilivyokuwa Agost 2015,''anaeleza.

Pia amesema thamani ya shilingi inatafsiriwa katika matumizi ya mlaji wa bidhaa mbalimbali ambapo shilingi ya Tanzania imeonekana kununua bidhaa na huduma zilezile katika vipimo tofauti tofauti.

''Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma imefikia shilingi 62 na senti 88 kwa Septemba 2015 kutoka Septemba 2010,''anaongeza.

Vilevile Mkurugezi huyo amesema farisihi za nishati na mafuta zimekuwa na mwenendo wa hali ya juu kwa kipindi chote zikilinganishwa na farihisi nyingine.

Amesema mfuko wa bei kwa kipindi cha mwezi mmoja umeongezeka kwa aslimia 0.1 ukiwa umechangiwa na baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula kama vile mkaa,pamoja na huduma za saluni.


No comments:

Post a Comment