Thursday, October 08, 2015

MAKAMU MWENYEKITI NCCR-MAGEUZI ASEMA YEYE BADO KIONGOZI

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ambapo alisema haridhishwi na utaratibu uliotumiwa na Mbatia wa kuitisha kikao ambacho kilihudhuriwa na viongozi wengine wakuu huku na kumvua madaraka wakati ni kinyume na Katiba ya Chama hicho.

Amesema sheria na utaratibu vilikiukwa kwani Katiba ya NNCR-Mageuzi ya mwaka 1992 toleo la 2014/ibara ya 27 (3)(C) inasema Makamu Mwenyekiti wa Taifa ataweza kuondolewa kwenye madaraka baada ya mapendekezo ya Halimasahauri kuu ya Taifa kwa azimio la mkutano mkuu wa Taifa,kwa zaidi ya nusu ya kura za wajumbe halali watakaodhuria na kupiga kura.

"Lakini pia kanuni za NCCR-Mageuzi toleo la mwaka 2012,umewekwa utaratibu wa kufuatwa kataika kumwajibisha kiongozi au mwanachama, kanuni hizi zinaitwa kanuni za nizamu na usuruhishi za Chama chetu,1996 kwa ujumla wake mashitaka ama malalamiko zidi ya mwanachama au kiongozi lazima yawakilishwe katika kikao cha utendaji cha ngazi husika kupitia kwa Katibu wa ngazi hiyo",ameeleza Mosore na kuongeza

"Mara baada ya kupokea malalamiko kikao husika kitamtaarifu muhusika juu ya malalamiko na kumtaka ajayajibu kwa maandishi katika muda wa majuma mawili".

Amesema lakini Mbatia amekiuka utaratibu huo wa Katiba na kanuni za Chama,mfano kikao anachodai kilikaa Septemba 22 mwaka huu hakikuwa kikao halali kwa mujibu wa Katiba na kanuni za Chama hicho bali kilikuwa ni kikao cha tathimini ya uchaguzi wa nchi ambao NCCR-Mageuzi inashiriki kinyonge kwa mwavuli wa UAKAWA.

"Hata kama kikao hicho kingekuwa halali bado kingekiuka haki ya msingi ya binadamu ya kupewa muda wa kujitetea,tena kanuni za Chama zinafafanua vizuri kabisa kwamba lazima mwanachama apewe majuma mwaili ya kujitetea kimaandishi ambayo mimi kama Makamu Mwenyekiti sikupewa kimsingi(Right to defend)",anasema Mosore na kuongeza

"Napenda kuufamisha umma na wana NCCR-Mageuzi wasiofahamu kwamba sina imani na kamati ya nidhamu na maadili ya Chama chetu kwa sababu nyingi ambazo ni,Kamati imeundwa na mWenyekiti mwenywe Mbatia,Mwenyekiti wake ni kaka yake aitwaye Thomas Nguma,Katibu ni shemeji yake aitwaye Tibajindela,huku wajumbe wakiwa ni shemeji yake aitwaye Dkt.Kahagwa na dada yake aitwaye Ndera.Je Kamati hii itaweza kutenda haki kwa mtu mwingine zaidi ya Mbatia?".Anahoji Mosore.

"Kwa tafsiri hiyo ya Katiba na kanuni za Chama chetu mimi ni Leticia Mosore mpaka sasa ni Makamu Mwenyekiti halali wa NCCR-Mageuzi (Bara)kwani ninatambulika na Katiba ya Chama,nilichaguliwa na mkUtano mkuu wa Taifa na wazifa wangu utakoma kuwa kiongozi kwa hiari ama kwa kufuata utaratibu kwa mujibu wa sheria na kanuni za Chama",Anaeleza.

Amesema anasikitishwa na ubakwaji wa demokrasia uliofanywa na Mbatia ambaye ndiye kiongozi wa juu wa Chama kwa maslahi binafsi bila kujali uhai na masalahi mapana ya NCCR-Mageuzi baada ya uchaguzi mkuu wa nchi wa mwaka huu Oktoba 25.

"Masikitikito yangu makubwa ni pale ninapoona kiongozi mkubwa kama Mbatia hadi sasa hajatembelea majimbo yetu ya ngome ya Chama huko Kigoma wala kampeni hazikufunguliwa katika majimbo yetu ya ngome badala yake ameenda kufungulia kampeni huko Vunjo.Je haoni anastahili kuyapa sapoti majimbo haya ya ngome?".Anahoji Mosore.

Amesema amekuwa akituhumiwa na Mbatia kuwa amewalaghai makimishina wa Chama hicho kwa kuwaita katika vikao vya kukihujumu Chama,na kudai kuwa kwa mujibu wa Katiba yeye akiwa kiongozi wa ngazi za juu ana mamlaka ya kukutana na wanachama,viongozi wa Chama,Makamishina na hata Katibu Mkuu mahali popote na kufanya mazungumzo.

Amesema kuhusiana na tuhuma za kuwa yeye amepanga njama za kumdhuru Mwenyekiti wake James Mbatia anaviachia vyombo vya usalama wa nchi vifanyie kazi na kuaidi kuwa atatoa ushirikiano wa dhati pale atakapohitajika kufanya hivyo.

"Lakini pia mimi kama Makamu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi(Bara) nashutumiwa na James Mbatia kuwa natumiwa na baadhi ya viongozi wa CCM Katika kukihujumu Chama chetu.Ndugu zangu, wanachama wa NCCR-Mageuzi na watanzania kiujumla,mwenye akili timamu apime na aelewe, Mbatia aliteuliwa ubunge viti maalumu na Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM,je kazi gani aliowafanyia CCM hadi akazawadiwa nafasi hiyo nyeti?Ninamuomba athibitishe na kuwataja viongozi wa CCM ninaoshirikiana nao",Alisema Mosore na kuongeza

"Mimi kama Mkamu Mwenyekiti wa NNCR-Mageuzi(Bara) narudia tena kutoridhishwa na mwenendo wa ushirikiano wa vyama vinavyounda UKAWA.Kwanini NCCR-Mageuzi ipewe mgawanyo wa majimbo machache ambayo ni 12, kati ya hayo majimbo 6 yameingiliwa na CHADEMA hivyo uhakika wa kushinda katika majimbo hayo ni mdogo sana kwani kura zitagawanyika na hali hii haikubaliki kwani inadhoofisha Chama chetu cha NNCR-Mageuzi"anaeleza.

No comments:

Post a Comment