Monday, October 05, 2015

MKUTANO WA KULINDA NA KUENDELEZA VITUO VYA BIASHARA TANZANIA WAFANYIKA LEO DAR.

.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipitia baadhi ya nyaraka alizokabidhiwa  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia, John Mngodo(kulia),   wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kulinda na kuendeleza Vituo vya Biashara Tanzania, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Okt 5, 2015.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya kufungua Mkutano wa Kulinda na kuendeleza Vituo vya Biashara Tanzania, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serenaleo.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wa Kulinda na kuendeleza Vituo vya Biashara Tanzania, baada ya ufunguzi huo.

  Baadhi ya washiriki na wadau waliohudhuria mkutano huo wa Kulinda na kuendeleza Vituo vya Biashara Tanzania, uliofunguliwa leo kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo, mara baada ya ufunguzi rasmi.(omr)


 WATAALAMU na wadau mbalimbali wamekutana nchini kwa ajili ya kujadili jinsi ya kuwawezesha wafanyabiashara kuboresha na kuendeleza biashara zao na kutambulika kimataifa.

Majadiliano hayo yalilenga kupanua vituo vitakavyowaweka pamoja vijana na  kuwapa ujuzi  wa namna ya kuanzisha biashara na kuziendeleza  ili kujikwamua  na umasikini kupitia fursa mbalimbali.

Makamu wa Rais Dkt.Gharib Bilali, amesema hayo leo wakati akifungua mkutano wa kulinda na kuendeleza vituo vya biashara ulioandaliwa na kampuni ya Property International ltd hapa nchini na Karat-18 ya Ureno.

Dkt.Bilali amesema wadau kutoka taasisi za umma na sekta binafsi wamekutana ili kupeana ujuzi,utaalamu na uzoefu  na kupanua vituo hivyo ili kuongeza ajira nyingi hasa kwa vijana wanaomaliza vyuo.

"Vijana wanaomaliza vyuo vikuu ni wengi na wanajikuta wakihangaika kutokana na kukosa ajira matokeo yake wanaishia kuzunguka na vyeti  bila kupata kazi lakini kampuni hizi kutoka Tanzania na Ureno watashirikiana kuweka vituo na kuhakikisha shughuli za kibiashara zinaongezeka kutokana na wingi wa watu,"amesema Dkt.Bilali.

Pia amesema vijana ndio taifa kubwa na lenye nguvu hivyo wakiwezeshwa kujiajiri na kutumia fursa walizonazo wataondokana na tatizo la ajira ambazo ni chache kutokana na kuongezeka kwa watu nchini.
"Miji inaendelea kukua na watu wanaongezeka kila siku mfano mwaka 2014 kulikuwa na watu bilioni 3 lakini kadri muda unavyokwenda wanaongezeka mpaka bilioni 5 hivyo wao wana uwezo  na ubunifu watasaidia katika suala la biashara kwani taifa ni kazi,"anaongeza.

Naye Katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano,sayansi na teknolojia,John Mngondo, amesema wataalamu hao watasaidia kuboresha miji na kupunguza idadi ya watu wanaoishi katika makazi yaliyojengwa kiholela.

Amesema itawasidia wafanyabiashara kuwa na maeneo maalumu yenye huduma zote za kibiashara ili kupunguza idadi ya watu kufuata huduma mijini na kupunguza misongamano.

"Tunaona mambo haya ya kuwa na makazi yaliyojengwa kiholela watu wanavyopata tabu hasa katika kipindi cha mvua nyingi hupoteza mali na kushindwa kufanya biashara zaao kutokana na mafuriko,"amesema Mngondo.


No comments:

Post a Comment