Wednesday, September 30, 2015

DC PAUL MAKONDA AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZA KATIKA GEREJI YA WACHINA NA KIWANDA CHA MAFUTA NA SABUNI, AKUMBANA NA CHANGAMOTO ZA KAZI ALILIA WAFANYAKAZI WAPATE MIKATABA.

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wafanyakazi wa Gereji ya Spring City Enterprises inayomilikiwa na raia wa China iliyopo Mikocheni B Mlalakuwa  Barabara ya Mwai Kibaki Dar es Salaam leo, alipofika kusikiliza malalamiko yao mbalimbali yakiwemo ya kutokuwa na mikataba ya kazi licha ya kuwa kazini kwa zaidi ya miaka saba,hicho ni  kitambulisho dhaifu wanavyotumia wafanyakazi hao ambacho hakiwezi kutumimika kumuwekea mtu dhamana na shughuli mbalimbali.

 
 DC Makonda (kulia), akiangalia bomba la maji wanayotumia wafanyakazi hao kwa kunywa. Hata hivyo wafanyakazi hao walilalamikia maji hayo kuwa si salama kwa kuwa yanatoka eneo la chooni.
 Kiongozi wa gereji hiyo, Mr Yu Viangqian (kushoto), akizungumza na wanahabari kuhusu madai ya kuwanyanyasa wafanyakazi wa kitanzania na kutokuwa na mikataba
 Ofisa Uhamiaji wa Wilaya ya Kinondoni, Evarist Mlay akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio baada ya kuwepo madai ya baadhi ya wachina kuishi nchini kinyemela.
Sehemu ya gareji inayolalamikiwa







No comments:

Post a Comment