Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi kutoka
Umoja wa Nchi za Ulaya, Judith Sergentine (kushoto) na Balozi wa Umoja wa Nchi
za Ulaya Tanzania, Filiberto Cebregondi, wakati walipofika ofisini kwake Ikulu
jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuwasili nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akiendelea na mazungumzo na Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi kutoka Umoja
wa Nchi za Ulaya, Judith Sergentine (wa tatu kulia kwake) na Balozi wa Umoja wa
Nchi za Ulaya Tanzania, Filiberto Cebregondi, (katikati yao) wakati walipofika
ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Sept 30, 2015 kwa ajili ya
kujitambulisha baada ya kuwasili nchini.
Baadhi ya watu walioongozana na Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi kutoka Umoja
wa Nchi za Ulaya,Judith Sergentine,wakifuatilia maongezi hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malawi,
Victoria Mwakasege, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam,
leo Sept 30, 2015 kwa ajili ya kumuaga rasmi akienda kuanza kazi nchini Malawi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini
Malawi, Victoria Mwakasege, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini
Dar es Salaam, leo Sept 30, 2015 alipofika kumuaga rasmi akienda kuanza kazi
nchini Malawi.(picha na OMR).
No comments:
Post a Comment