Tuesday, July 21, 2015

RAIS WA ZAMANI WA CHAD ASHTAKIWA SENEGAL


Rais wa zamani wa Chad Hissene Habre (Pichani Kushoto) atafikishwa mahakamani nchini Senegal kwa makosa ya uhalifu dhidi ya Binadamu,ukatili dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita

Umoja wa mataifa umemshtaki kiongozi huyo ambapo Bw Habre anashutumiwa kwa kuhusika na vitendo vya ukatili na mauaji ya maelfu ya watu wakati wa enzi ya utawala wake kuanzia 1982 hadi 1990 shutuma ambazo anazikanusha.

Kesi hiyo inafuatia miaka 25 ya kampeni za kumfikisha mbele ya sheria ambapo wengi miongoni mwa watu wanaodaiwa kuwa ni waathirika wa uhalifu uliotekelezwa na Bw Habre wamekuwa wakitoa wito wa kufunguliwa mashtaka dhidi yake tangu alipopinduliwa mamlakani na kukimbia uhamishoni nchi senegal 1990.

Mnamo mwaka 2005 mahakama ya Ubelgiji ilitoa kibali cha kumkama,ikidai kuwa na haki ya kimataifa ya kufanya hivyo,lakini baada ya mazungumzo na umoja wa afrika AU iliomba senegal kuendesha kesi dhidi ya Bw Habre kwa niaba ya Afrika.









No comments:

Post a Comment