Tuesday, June 09, 2015

BREAKING NEWS: MZEE KANKAA WA JUMBA LA DHAHABU AAGA DUNIAMsanii wa Bongo Muvi, Juma Kankaa 'Mzee Kankaa' amefariki dunia jana nyumbani kwake Tandale Chama,Dar es Salaam.

Msanii huyo ambaye aliwahi kuigiza michezo kama Jumba la Dhahabu na Milosis, amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa Kiharusi.

Ahmed Olutu 'Mzee Chilo' msanii wa filamu nchini amesema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa msiba huo kwani ni mtu ambaye alikuwa amemzoea sana na ambaye alishawahi kufanya naye kazi kwa kipindi kirefu.

"Tunasema ni mapenzi ya Mungu leo kuondokewa na msanii mwenzetu, lakini sote tupo njia moja leo yeye na kesho sisi ila tupo katika maumivu makubwa na kipindi kigumu kwetu kama wasanii," alisema Chilo.

Mzee Kankaa amezikwa leo nyumbani kwake Tandale Chama,Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment