Monday, August 04, 2014

KIM KARDASHIAN ANAINGIZA SHILINGI BILION 1 KWA SIKU, SOMA HAPA ANAPATAJE

Kim Kardashian anafahamika kwa kutokuwa na shughuli ya kufanya, sasa hivi amanzisha mchezo unaomwingizia Dola za Kimarekani 700,000 (sawa na shilingi za Kitanzania 1,160,950,000 ) kwa siku, wachezaji wanatakiwa kufanya nini? Jibu ni hakuna…

Mchezo wenyewe unapatikana bure... ndio download bure, ispokuwa sasa, kucheza utatumia hela za kweli kwenye vitu ambavyo huwezi kuvishika kama nguo, nywele nakadhalika, ambayvo mwishowe unapata katuni kama ya Avatar. Kwa jinsi unavyopata point nyingi ndivyo unavyozidi kupanda ngazi, jambo ambalo ndio lengo la mchezo wenyewe.

Kwa mujibu wa mdadisi kutoka katika kampini ya Cowen and Company ya nchini Marekani, Doug Creutz, kama mauzo yataendelea katika hali iliyopo, mchezo huo utavuka zaidi ya Dola za Marekani milioni 200(sawa na shilingi za Kitanzania 331,700,000,000) kwa mwaka wa kwanza pekee

Kwa mujibu wa mtandao wa CNN Money, Jambo hilo litafanya "Kim Kardashian: Hollywood" kuwa kati ya washindani wakubwa wanaouza michezo ya kwenye simu kwa kiasi kikubwa duniani kama vile Candy Crush.

Creutz anasema inakisiwa kuna michezo ye kwenye simu kama 7 tu ambayo inatengeneza pesa nyingi kwa sasa, na mchezo wa Kardashian umeingia katika tano bora ya app inayotumika kutoka Apple Store.

No comments:

Post a Comment