Monday, August 04, 2014

NEWS: TETEMEKO LA ARDHI LAUA WATU 380

Wafanyakazi wa Uokoaji nchini China wanaendelea kujitahidi kufikia eneo la lilipigwa na tetemeko la ardhi katika jimbo la Yunnan siku ya jumapili na kuua watu zaidi ya mia tatu na themanini.

Kikosi cha dharura kinajaribu kukarabati barabara zilizoharibiwa ili kuwezesha usafiri katika maeneo yaliyopata mvua kubwa na kusababisha mmomonyoko wa ardhi.

Maelfu ya watu waliodhurika na tetemeko hilo wapo katika maeneo ambayo ni vigumu kufikiwa na mamlaka zinazohusika. Shuhuda mmoja amesema karibu theluthi mbili ya nyumba zimeharibiwa katika kijiji chao.

Maelfu ya mahema na vitanda vya dharura vimepelekwa katika eneo hilo liloathirika na maelfu ya wafanyakazi wa idara ya dharura watumwa kusaidia kazi ya uokoaji.(BBC)

No comments:

Post a Comment