Thursday, June 19, 2014

MUME WA FLORA MBASHA ATOLEWA MAHABUSU KWA DHAMANA

Mfanyabiashara ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za injili ambaye ni mume wa Flora, Emmanuel Mbasha anayetuhumiwa na kukabiliwa na kesi ya ubakaji yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Emmanuel Mbasha aliruhusiwa na mahakama ya Wilaya ya Ilala, baada ya kutimiza masharti hayo leo asubuhi katika mahakama hiyo, ambapo moja ya masharti hayo ni wadhamini wawili ambao wote ni wafanyakazi wa taasisi inayotambulika kisheria.


Kesi ya Bw. Mbasha inatarajiwa kunguruma tarehe 17 Julai, mwaka huu ambapo mwendesha mashtaka alidai kuwa ushahidi wote umeshakamilika.

Emmanuel Mbasha alifikishwa mbele ya Hakimu Willbaforce Rwago, chini ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Nassoro Katuga katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala june 17 mwaka huu kwa madai kuwa Mbasha alitenda kosa la ubakaji tarehe 23 Mei mwka huu huko Tabata Kimanga, jijini Dar Es Salaam.




Hata hivyo Bw. Mbasha alikana shitaka hilo linano husiana na kumbaka msichana wa miaka 17 anayedaiwa kuwa ni mdogo wa mke wake ambaye pia ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili, Flora Mbasha. Bw. Mbasha alipelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.


No comments:

Post a Comment