Friday, May 30, 2014

SIMBA NA YANGA ZAPATA ACCOUNT MAALUM BENKI YA POSTA

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Vijana na Michezo, Juma Mkamia amelaani viongozi wanaowania nafasi za uongozi wa klabu ya Simba kuleta mgogoro jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya soka hapa nchini.

Mkamia ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa Benki ya Posta ilipokuwa ikizindua huduma ya account maalum kwa timu ya Simba na Yanga. Alisema viongozi wanaogombea ubosi ndani ya klabu ya simba wanatakiwa wawe makini kwa kuwa wao ndio chanzo cha migogoro katika klabu.

Aidha alisema simba kwa sasa ipo katika mgogoro mkubwa wa viongozi wanaowania nafasi za uchaguzi kitendo ambacho hakitaleta tija katika mpira wa miguu hapa nchini.

Pia alisema wanapoendeleza migongano hakuna kampuni zinazoweza kujitokeza kusaidia kwa kuwa hawatapenda kuona wanaingia katika vilabu vyenye matatizo jambo ambalo sio zuri.

“mnalalamika na wadhamini hali ya kuwa kila siku kunakuwa na migongano,”alisema Mkamia

Kwa upande wake Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuph Manji alisema amefarijika kuona kwamba wameingia makubaliano na bank ya Posta itakayosaidia maendeleo ya klabu yako. Alisema kila mwanachama anatakiwa kuwa na account itakayoingia shilingi 250 kwa wiki ambapo kwa mwezi hatakuwa amechangia kiasi cha shilingi 1000.

Naye Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage alisema ataondoka klabuni hapo akiwa amewaacha vizuri ikiwemo kupata uwanja wa mazoezi mwezi ujao. “Nitawaacha Simba katika wakati mzuri ikiwa Bank ya Posta wameingia na uwanja nitakabidhi mwezi ujao” alisema Rage

No comments:

Post a Comment