Friday, May 30, 2014

SEMINA MAALUMU KWA WANAKARATE WENYE MKANDA MWEUSI NA KIJANI

Chama cha mchezo wa karate hapa nchini (TASHOKA) kinatarajia kuendesha semina ya wazi kwa wanakarate wenye darajala wa mkanda wakijani na mweusi itakayofanyika juni 14 hadi 15 katika viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa TASHOKA , Philip Chikoko alisemakuwa Semina hiyo muhimu itashirikisha wanakarate kutoa mikoa yote ya Tanzania yenye lengo la kujiandaa kushiriki kwenye mashindano ya kanda ya tano yanayotarajiwa kufanyika mjini Addis ababa nchini Ethopia julai mwaka huu.

Alisema semina hiyo itatolewa bure kwa kufadhiriwa na tawi la Tanzania la Shirikisho la Karate la kimataifa hivyo ameomba wanakarate kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha semina hiyo.
“wanakarate wajitokezekwa wingi ili tupate wachezaji wazuri wa kushiriki michuano hiyo muhimu itakayolitangaza taifa, “alisema Chikoko.





No comments:

Post a Comment