Baada ya wanachama wa klabu ya Simba kufunga mlango katika ofisi za klabu hiyo kwa kile wanachodai kuenguliwa kwa Michael Richard Wambura hawakuridhishwa Katibu Mkuu wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kuwa hatoingia tena katika klabu hiyo hata kama wakifungua.
Tukio hilo limetokea baada ya kuenguliwa Wambura na kamati ya Uchaguzi, uchaguzi unaotarajiwakufanyika juni 29 mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Kamwaga alisema kuwa walichokifanya wanachama ni uhuni na kwa upande wake hakuridhika angeweza kujiuzuru hata leo lakini kutokana na jukumu alilopewa la kujenga uwanja wa Simba maeneo ya Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
“nashinda kujiuzuri kwa sasa kutokana na majukumu ya ujenze wa uwanja lakini uwanja ukimalizika nitaachia ngazi kwani sioni sababu ya kuendelea na Simba,”alisema Kamwaga
Aidha alikanusha taarifa za kufurahia kuenguliwa kwa Wambura kwa kuwa yeye ni mjumbe wa kamati ya utendaji hivyo aoni sababu ya kushangilia hali ya kuwa taarifa za kuenguliwa kwake anazifaham siku nyingi.
Alisema wanachama hawatakiwa kufanya walivyofanya kwa kuwa Wambura ameamu kufuata ngazi na utaratibu kupitia kamati ya Rufaa hivyo walitakiwa kuiachia kamati ifanye kazi zake kwa utaratibu unaotakiwa.
Lakini pia Kamwaga amesikitishwa nataarifa za kuiba nyaraka klabuni hapo kwa kuwa haoni kama ni suala la msingi kufanya hivyo wakati hajasimama kwa kumgombea yeyote anachoamini kila kiongozi anamfaa katika Simba.
No comments:
Post a Comment