Friday, May 30, 2014

BREAKING NEWS: TAIFA STARS YAHUJUMIWA JIJINI HARARE, ZIMBABWE (SOMA HAPA)

Katika hali isiyo ya kawaida wachezaji wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, wamefungiwa vyumba vya hoteli waliyofikia mjini Harare, Zimbabwe, ambapo wapo kwa ajili ya mchezo wa marudiano na wenyeji kesho hatua za awali za Kombe la Mataifa ya Afrika. 

(KUSHOTO:Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa Stars wakiwa katika ukumbi wa reception wakisubiri hatma yao jioni hii, baada ya kunyimwa funguo za vyumba vyao vya kulala)

Stars iliwasili nchini Zimbabwe jana salama salmini na kufikia katika Hoteli ya Best City Lodge mjini Harare, wakati wachezaji wanarejea kutoka mazoezini jioni hii ndipo walipopigwa na butwaa baada ya kunyimwa funguo za kuingia vyumbani mwao.

Katika hali kama hiyo ambayo inaweza kutafsiriwa kama ni fitna za mchezo, chanzo chetu cha habari kilichoko jijini Harare, kilituambia kuwa sababu kubwa inayodaiwa ni kwamba hawajalipia malazi katika hoteli hiyo tangu wamefika. 
Kama wanavyoonekana pichani wakiwa katika eneo la mapokezi, viongozzi wa TFF mpaka tunakwenda mitamboni wanahaha kutafuta jawabu la tatizo hilo huku wakiwa wamechanganyikiwa na tukio hilo.

Stars inatarajiwa kucheza na Zimbabwe siku ya jumapili, ikiwa ni mechi ya marudiano ya hatua ya kwanza ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco.

Katika mchezo wa kwanza Tanzania ilishinda 1-0 ikiwa ni wiki moja iliyopita katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Stars imejiweka katika mazingira ambayo itahitaji ushindi au kutoa sare ili kusonga mbele.


No comments:

Post a Comment