Tuesday, April 01, 2014

ZIARA YA RAIS KIKWETE LONDON KATIKA PICHA



Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe kuzindua rasmi mpango wa bima ya afya na maafa wa WESTADI wa mfuko wa Jamii wa NSSF jijini London, akiwa na Mkurugenzi wa NSSF Dkt Ramadhani Dau na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya mfuko huo Bw. Abubakar Rajabu (kushoto) . Mwenye miwani kati ni Bw. Aboubakar Faraji aliyekuwa mwongoza sherehe wa siku hiyo ambapo Dkt Kikwete alikutana na kuzungumza na Watanzania waishio Uingereza.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Bw. Hague alipomtembelea ofisini kwake jijini London kwa mazungumzo Machi 31, 2014

Chini: Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron alipomtembelea ofisini kwake 10 Downing Street jijini London kwa mazungumzo Machi 31, 2014,




Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron alipomtembelea ofisini kwake 10 Downing Street jijini London kwa mazungumzo Machi 31, 2014


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wafanyabishara wakubwa na wawekezaji wa Uingereza aliokutana nao katika mkutano wa biashara na uwekezaji katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola jijini London Machi 31, 2014




No comments:

Post a Comment