Tuesday, April 01, 2014

MAJANGILI WA MENO YA TEMBO 6 WAKAMATWA NA SMG NA RUNDO LA RISASI

Arusha.

Wizara ya maliasili na utalii imetangaza kukamatwa kwa meno 53 ya tembo yenye jumla ya kilo 169.7na silaha moja ya kivita aina ya SMG na magazine tatu pamoj na majangili sita katika wilaya ya Manyoni mkoani Singida

Akitangaza mbele ya waandishi wa habari mkoani Arusha jana Waziri wa maliasili na utalii Mh.Lazaro Nyalandu alisema tukio hilo lilitokea jana katika kijiji cha kiombo Wilaya ya manyoni ambapo tembo 26 wameuwawa na majangili katika maeneo ya hifadhi za Rungwa na Kizigo

Waziri Nyalandu alisema kuwa jumla ya majangili 6 wameshikiliwa chini ya ulinzi mkali katika kituo cha polisi cha Manyoni ambapo walikutwa na meno ya tembo 53,silaha ya kivita moja na magazine tatu.

Nyalandu alisisitiza kuwa pamoja na changamoto kubwa iliyopo dhidi ya ujangili serikali imeazimia kuwasaka na kuwakamata majangili na washirika wao popote walipo huku akidai kuwa zoezi la kuwasaka ni la usiku na mchana

Aidha alisema kuwa msako unaendelea kuwasata wauwaji wa tembe 26,huku akiwaomba wananchi wenye taarifa kuhusu uhalifu watoe ushirikiano wao kwa askari wa wanyama pori,jeshi la polisi na vyombo vya usalama

Pia alitoa pongezi zake kwa mkurugenzi wa wanyama pori na kikosi chake dhidi ya ujangili kanda ya kati Manyoni na kikosi kazi maalum(Task force)kwa weledi na kujituma kwao ambapo imefanikisha kukamatwa majangili hao na meno ya tembo


No comments:

Post a Comment