Wednesday, April 16, 2014

MAAJABU: MTOTO MWENYE GAMBA LA KOBE AFANYIWA UPASUAJI


* AFUKUZWA SHULE, ATENGWA SABABU YA HALI YAKE


Didier Montalvo kutoka Colombia vijijini, amepata tatizo ambalo limesababisha magamba kuota katika sehemu mbalimbali za mwili wake katika kasi ya ajabu. Matokeo ya ugonjwa ni magamba yaliyoota kuwa makubwa kiasi cha kuziba mgongo wote.

Kijana huyo alipewa jina la “Kobe mtu” na wenzie kutokana na magamba hayo kuwa makubwa na kusababisha kuonekana kama jumba la kobe. Imedaiwa kuwa mama yake Didier alibeba ujauzito siku ya kupatwa kwa mwezi na kuaminika kuwa hiyo ni kazi ya shetani.

Kwa sababu hiyo alitengwa na watoto wenzie shuleni na kuzuiwa kwenda shule. Mwingereza mmoja daktari wa upasuaji aliposikia taarifa hizo, alifunga safari kwenda Bogota ili akamfanyie upasuaji kuondoa magamba hayo.

Didier alikuwa na umri wa miaka 6 alipofanyiwa upasuaji. Alifanikiwa na magamba hayo yaliondolewa. Baada ya upasuaji, Didier sasa anakwenda shule na kuishi maisha ya kawaida akiwa na furaha.



TAFADHALI ANDIKA MAONI YAKO CHINI. . .


No comments:

Post a Comment