Thursday, April 17, 2014

HAWA NDIO WASANII WA HIPHOP MATAJIRI KULIKO WOTE DUNIANI, ONA KWANINI

Jarida la Forbes limetoa orodha ya wasanii wa musiki wa HipHop ya wasanii watano wenye utajiri mkubwa zaidi duniani na orodha hiyo inaongozwa na Pdiddy mwenye utajiri wenye dhamani zaidi ya dola za kimarekani milioni 700 yenye ongezeko la dola milioni 120 mwaka jana.

Sean "Diddy" Combs -$700 Million
Andre "Dr. Dre" Young" - $550 Million
Shawn “Jay Z” Carter -$ 520 Million
Bryan “Birdman" Williams
Curtis "50 Cent"Jackson -$140 Million

Fedha nyingi za Dr.Dre zinatokana na mauzo ya headphone zake zinazojulikana kama ‘Beats By Dre’ zikiwa na mauzo yanayoripotiwa kuwa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 1 na yanaendelea kupanda.

Utajiri wa msanii mkongwe wa HipHOp Jay Z hivi karibuni umeongezeka kutokana na Roc Nation, kampuni yake ya muziki na inayomiliki wasanii kadhaa ambayo hivi karibuni imeongeza uwakala wa michezo.

Utajiri wa Birdman unafikia kiasi cha dola za kimarekani milioni 300 na kuchanganya na utajiri wa mdogo wake Ronald”Slim”, waanzilishi wa kampuni ya muziki ya Cash Money Records miongo miwili iliyopita, waliingia mkataba na msanii Drake, Nicki Minaj na Lil Wyne Williams.

Msanii mwingine 50 Cent utajiri wake ni zaidi ya dola za kimarekani milioni 100, utajiri unaotokana na mauzo ya maji yenye vitamin mwaka 2007.

TAFADHALI CHANGIA MAWAZO YAKO HAPO CHINI


No comments:

Post a Comment