Thursday, April 17, 2014

JAMBAZI LAKATWA MKONO KISHA WANING'NIZWA MTAANI, TAHADHARI; PICHA YAWEZA KULETA USUMBUFU



Hii imetokea hivi karibuni, kwa mujibu wa taarifa ni kwamba jambazi moja alivamia na kumshambulia kijana mmoja nyumbani kwake muda wa saa kumi alfajiri, akampiga kijana huyo na kumlazimisha kutoa vitu vya dhamani alivyonavyo.

Jambazi hilo huku likiwa na hasira likamtishia kumpiga risasi kama asingetekeleza amri yake haraka, hata hivyo inaelekea jambazi hilo halikuwa na bahati kwani kijana huyo alipopata fursa aliokota kipande cha kioo na kufanikiwa kumkata mkono na hatimaye jambazi hilo likakimbia huku likiwa limejeruhiwa.

Hata hivyo hakufika mbali sana, wakazi wa eneo hilo wanasema walilikuta jambazi hili mtaa wa pili likiwa hoi. Tukio hilo limetokea nchini Nigeria, ambapo mkono wa jambazi hilo umening’inizwa mtaani kama picha inavyoonesha.TAFADHALI CHANGIA MAONI YAKO HAPO CHINI. . .

No comments:

Post a Comment