Thursday, April 17, 2014

UJUMBE WA KUSIKITISHA WA MTOTO KWA MAMA YAKE KATIKA FERI ILIYOZAMA KOREA KUSINI JANA

Haya ni maelezo yenye kuumiza sana yanayodaiwa yalitumwa kama ujumbe mfupi wa simu na kijana mmoja kwa mama yake wakati kivuko cha Korea Kusini kikizama polepole baharini.

Mama akajibu kwa maneno ya upendo na kuonesha kujali, lakini hakupata majibu yoyote. Pichani ni baadhi ya jumbe hizo na majibizano baina ya kijana kutoka katika kivuko kilicho kuwa kinazama na mama yake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyorushwa na televisheni ya CBC News, kijana huyo ni mmoja wa abiria wanaokisiwa kuwa 475 waliokuwepo katika chombo hicho kilichoanza kuzama jumatano (jana) kusini mwa Korea Kusini.
Mpaka taarifa hizi zinatolewa watu sita walikuwa tayari wameripotiwa kupoteza maisha katika ajali hiyo, huku watu 290, wengi wakiwa ni wanafunzi wa sekondali ya juu wakielekea katika ziara ya masomo hawajaweza kupatika kwa mujibu wa AP (Associated Press).

Mama mmoja analia wakati yeye na wengine wakiwa wanatafuta majina ya watoto wao katika orodha ya waliookolewa katika pantone iliyozama kusini mwa pwani, Shule ya Danwon huko Ansan, Korea Kusini, jana tarehe 16/04/2014.

Haijajulikana kama kijana aliyetuma ujumbe kwa mama yake kama ni mmoja wa waliookolewa au la. Lakini katika taarifa ya kukatisha tamaa, taarifa ya Andrew Salomon wa CNN ilisema “watoto wengine pia walituma ujumbe mfupi wa simu(SMS) kwa wazazi wao wakati kivuko hicho kinaanza kuzama.


“Baba siwezi kutoka,” msichana mdogo aliripotiwa kutuma ujumbe kwa baba yake. “Meli imegeuka sana.”
Salmon aliripoti kuwa pantoni hiyo ilichukua zaidi ya saa mbili kuzama kabisa. “Kulikuwa na, kwa maana kwamba, muda wa kutosha kwa watu kutafuta jawabu la namna ya kutoka” alisema. Kwa sababu hiyo, CNN iliripoti kuwa abiria waliokuwa katika meli hiyo ambao inadaiwa walijaa zaidi upande mmoja, waliambiwa kubaki wakisubiri msaada wa kuokolewa.

“Tuliambiwa kuwa tubaki mahali ulipo, kwa hiyo tukabaki” mmoja wa waliookolewa alikaririwa akisema kwa mujibu wa CNN. “Lakini baadae, kina cha maji kikaanza kupanda. Hivyo tukabaki wenyewe. Watoto wanapiga makelele kwa hofu, wakiomba msaada.” Sababu ya pantoni hiyo kuzama haijajulikana bado.

TAFADHALI ANDIKA MAONI YAKO HAPA CHINI . . .


No comments:

Post a Comment