Mchungaji huyo ni mchungaji wa kanisa la wokovu lijulikanalo kama Vision Church (Kanisa la Maono). Msemaji wa polisi Nairobi Anthony Kibuchi alisema bomu hilo la kutengeneza lilikuwa tayari kwaajili ya kulipuka.
“Naweza kudhibitisha ni bomu lililotengenezwa kwa mkono na tumekamata watu wawili, ikiwa ni pamoja na mchungaji. Lakini hatujajua ni wapi wangetumia kifaa hicho hatari” Kibuchi aliliambia gazeti la Standard kwa njia ya simu juma pili iliyopita. Bomu hilo limetengenezwa kwa kemikali hatari, lina uzito wa kilogramu 1, likiwa pia na kifaa cha kulipulia. Alieleza Kibuchi.
Anasema alihitaji msaada kutoka kwa mtu ambaya anafanya kazi katika machimbo ya mawe jijini il amsaidie kutengeneza bomu pamoja na kifyatuzi chake. “bado tunaendelea kumhoji mchungaji na mwenzie kabla hatujawafahamisha zaidi. Tumelidhibiti tukio hivyo hakuna sababu ya kutaharuki” alisema Kabuchi.
Vyanzo vimeeleza kuwa timu iliyomkamata mchungaji inategemea kuwakamata wengine zaidi. Wataalamu wamesema kuwa bomu lilikamatwa lina uwezo wa kushusha gorofa au kusababisha hasara kubwa.
Mashahidi wamesema, maofisa kutoka Kitengo Maalumu cha Kuzuia Uhalifu walimkamata mchungaji na mwenzie katika makutano ya barabara ya Kiambu/Runda kwa bunduki saa kumi jioni. Watuhumiwa walipelekwa katika vituo tofauti vya polisi wakati wengine wanaendelea kutafutwa.
TAFADHALI ANDIKA MAONI YAKO HAPA. . .
No comments:
Post a Comment