Iringa
Katika mchakato wa kukuza utalii wa ndani Mkoa wa Iringa una mkakati wa kuanzisha maadhimisho ya siku ya mkwawa itakayojulikana kama MKWAWA DAY
Hayo yamebainishwa jana na ofisa wanyamapoli ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa Faustine Majuto wakati akizungumza na majira ofisini kwake juu mkakati wa kukuza utalii wa ndani.
Alisema kuwa lengo la mkoa kuanzisha Mkwawa day ni kuhamsisha utalii na kukuza utamduni wa ndani kwa wazaliwa na wageni wanaopenda utalii
Aidha alisema kuwa faida zitokanazo na utalii kwa wakazi wa Iringa ni pamoja na kukua kwa uchumi kwa kuuza vitu vya asili, kudumisha utamaduni na kuongezeka kwa huduma za kifedha
"nina uhakika tukikuza utalii wetu wa ndani uchumi utakua kwani watu wengi watatengeneza vivutio kama vikapu vya asili vya kubebea unga mikeka, mabegi na mikoba ya asili, vigoda mavazi ya asili kama aliyo vaa chifu mkwawa wasanii watatoa video zao zenye nyimbo na ngoma za tamduni”
Faida zingine ni kutunza utamaduni wa zama za mambo ya kale kama vile silaha za jadi, mavazi ya kihehe na kutembelea makaburi ya zamani.
Pamoja na faida hizo FAUSTENE alisema changamoto wanazokabiliana nazo katika kukuza utalii
ni uhaba wa hoteli bora za kutosha,uchache wawaongozaji watalii, na uelewa mdogo kwa kuhusu
utalii
Changamoto nyingine ni ujangiri uliokithiri hasa kwa wanyama aina ya tembo’’tuna tatizo kubwa sana la ujangili hasa wa tembo kiukweli unahatarisha sana usalama wa wanyamapori kama mnavyosikia kila siku katika vyombo vya habari ujangili wanaofanyiwa tembo sisi kama wahusika wakubwa katika usalama wao tunaumia sana”alisema.
Hata hivyo aliwataka wananchi wa mkoa wa Iringa kutoa taarifa kwa vitendo vyovyote vinavyojitokeza vyakijangiri ili kuhakikisha vitendo hivyo vinadhibitwa kikamilifu kabla havijafanyika
Aidha alitoa wito kwa wananchi kutembelea katika hifadhi za kale mkoani Iringa kama vile Isimila, Kalenga, daraja la mungu pamoja na mbuga ya Mbomipa zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya Iringa
No comments:
Post a Comment