Wednesday, April 23, 2014

HII INATISHA JAMANI DUH: WATOTO 800 WAMELAWITIWA. . ., NDIO 800, SOMA HAPA

Zaidi ya watoto 800 wamelawitiwa kwa mwaka jana na watoto kumi kubakwa na wazazi wao taarifa ya tafiti ya kituo cha Haki za Binadamu imebaini hivyo na kutaka juhudi zaidi kufanyika katika kukabiliana na vitendo vya ukatili.

Hayo yalisemwa Dar es salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dokta Helen Kijo-Bisimba wakati wa uzindua wa taarifa ya haki za Binadamu Tanzania ya mwaka 2013

Alisema kumekuwa na matukio ya kukithili kukatizwa kwa haki ya kuishi kwa njia mbalimbali zaidi kwa mwaka huo ambapo matukio ya mauaji ya kutisha kwa kujichukulia sheria mkononi kwa wananchi,polisi na vikongwe,ukatili wa wanawake na watoto ambapo ya zaidi ya 800 wamelawitiwa na kumi kubakwa na wazazi wao.


“katika ripoti hii tumebaini zaidi ya watoto 800 wamelawitiwa na kumi kubakwa na wazazi au walezi wao sambamba na mauaji ya albino,ajali za barabarani na sheria mkononi kwa madereva bodaboda ambapo pia katika sura ya tisa ya ripoti tumeeleza tatizo la rushwa linavyochangia ukiukaji wa haki ya elimu na afya”alisema

Alisema katika tafiti za taarifa hiyo wamebaini matukio 10 lakini yapo matatu makuu yaliyopelekea ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo ya kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyoitoa Bungeni juu ya wakaidi wapigwe tu na polisi hali iliyochechea mauaji na ukiukwaji wa haki kwa kiasi kikubwa katika Oparesheni mbalimbali ikiwemo ya Kimbunga na Tokomeza.

Dkt Kejo-Bisimba alisifu ushirikiano uliopo kati ya kituo hicho na Serikali katika kuchangia ufuatiliaji wa haki za binadamu nchini ambapo imepelekea kuingia mikataba mbalimbali ya kimataifa sambamba na ushirikiano mzuri na jeshi la polisi huku bado kukiwa na changamoto kubwa katika kupata taarifa katika sekta ya elimu.

Kwa upande wa Jeshi la polisi Mkurugrugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai,kamishna wa Polisi (CP) Isaya Mngulu alisema kufuatia taarifa hizo za haki za Binadamu zimekuwa zikilisaidia jeshi la polisi kutambua takwimu kuhusu hali halisi ya haki za binadamu nchini kwa bara na visiwani hatua inayopelekea kubaini kiwango cha ulinzi au ukiukwaji wa haki.

Alisema taarifa hizo pia zimekuwa zikiibua ,kuelimisha,kulinda na kutetea haki za binadamu nchini na kuwa chachu ya mabadiliko katika sera na sheria mbalimbali kwenye mfumo wa utawala sambamba na kuwa nyenzo ya kufundishia haki za binadamu katika maeneo mbalimbali ikiwemo vyuo,shule za sekondari ukufunzi wa wasaidizi wa sheria na waangalizi wa haki za binadamu.

“Tumebaini kupitia taarifa hiii kuwa kuna ongezeko kubwa ya ukiukaji wa haki za raia na haki za makundi maalum katika jamii hususani akina mama na watoto ,mauaji ya vikongwe kwa imani ya kishirikina pia imekuwa na kuenea kwa kasi nchini”alisema

Aidha aliwataka wananchi kujenga imani na jeshi hilo hasa katika utoaji wa haki kwa makosa ya jinai kwani dhamana ni haki ya kikatiba kwa kila mmoja.

Alisema kuwa kumekuwapo na mawazo potofu kuwa mtu akipelekwa kituo cha polisi na kuonekana mtaani basi ameachiwa kwa rushwa haliyakuwa dhamana ni haki ya mtuhumiwa yeyote ukiacha makosa ya jinai machache ikiwemo mauaji.

“ni muhimu kujenga imani na jeshi la polisi kwani katika utoaji wa haki kwa makosa ya jinai ukiachia makosa machache ikiwemo ya kuua katiba inatoa misingi ya kisheria ambayo inapaswa kufuatwa”alisema

Aliongeza kuwa elimu ya kutosha itapunguza kiwango kikubwa cha wananchi kujichukulia sheria mkononi hali ambayo kwa sasa inatisha katika kuongeza mauaji ya wasio na hatia hususani katika miji mikubwa.

TAFADHALI ANDIKA MAONI YAKO HAPA CHINI. . .


No comments:

Post a Comment