Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa
angalizo na onyo kwa vijana wa CCM ambao wako kwenye maandalizi ya kuanza
kufanya fujo zinazoratibiwa kimkakati kuharibu mchakato wa Katiba Mpya ili
kuwapatia ‘fursa’ watawala kuweka visingizio vya kuzuia harakati za UKAWA
kuuelimisha umma.
Taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari Jijini Dar es
Salaam jana na Kurugenzi ya mawasiliano ya Chadema na kusainiwa na Afisa
Utawala na Fedha Baraza la Vijana BAVICHA Bwana Daniel Naftal iliwataka CCM kutokujaribu wala kudiriki
kutekeleza hayo maagizo ya kuwashambulia wananchi kwenye shughuli zao
mbalimbali na viongozi wa UKAWA.
Alisema kuwa Katika hilo wameomba kuwa wazi, kuwa wako
tayari kusimama na kuwalinda viongozi wao.
Aliwataka wananchi kuungana na makundi mbalimbali katika
jamii, taasisi, asasi za kiraia na watu wengine mashuhuri ambao wameamua
kujitoa hadharani kusimamia maoni ya wananchi kama yalivyowasilishwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Mpya kwenye Rasimu ya Pili, ambayo inaeleza katika katiba
ya sasa, ibara ya 8 inayosema mamlaka ya kuongoza nchi yote yatatoka kwa
umma/wananchi.
Aidha pia alihimiza kutumia nguvu zote zilizojaa ushawishi
wa hoja na mbinu halali dhidi ya njama za aina yoyote zinazofanywa kupindua na
kuchakachua maoni.
“Leo pia tunaendelea kusisitiza kuwa hakuna kikundi chochote
kinaweza kujitwalia mamlaka ya kwenda kinyume au kupindua maoni ya wananchi
kwenye Rasimu ya Katiba Mpya, ambao ndiyo wenye hati miliki na nchi yao.”ni
wazi watawala wanataka kupola na kubaka demokrasia kwenye jambo nyeti kama hili
kwa manufaa ya CCM.
Alisema Bavicha kwa kushirikiana na vijana wengine
wenye machungu na Tanzania watashawishi, kuratibu na kusimamia hoja za msingi
katika kuhakikisha kizazi cha sasa na vingine vijavyo, vinanufaika na matunda
yatakayo andaliwa leo.
Alisema zimeanza kuonekana dalili za njama za wazi kabisa
zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia njia mbalimbali kutaka
kutengeneza hali ya taharuki na kuwatisha wananchi wasijenge hoja za kudai
maoni yao yaheshimiwe kwenye kuandika Katiba Mpya ya Tanzania.
“Njama hizo za kujenga hali ya hofu na kuibua sintofahamu
ambazo zimekuwa zikizungumzwa na viongozi waandamizi wa chama hicho,
zimeendelea kudhihirika tena baada ya chama hicho, kupitia kwa kada wake. Paul
Makonda, kutoa tamko la kuhamasisha vurugu na ‘kuanzisha’ vita, kwa nia ya
kuwatisha wananchi washindwe kudai katiba yao inayotaka kuporwa na CCM”alisema.
Naftal
alisema Kada huyo ambaye anajulikana ndani na nje ya chama chake kwa namna
alivyo mahiri wa kutumika kwa ajili ya maslahi binafsi ya watu au wakati
mwingine hata dhidi ya chama chake, kwa ajili tu ya kutetea tumbo lake, amekuwa
akitoa maneno ambayo kwa hakika yamezidi kuwachochea wananchi kujua kuwa CCM si
chama cha siasa tena, bali genge la wabaka demokrasia.
Alisema kutokana na Makonda kunukuliwa akitoa maagizo
kwa vyombo vya dola na vijana wanaounda jeshi haramu la CCM (Intarahamwe),
linalojulikana kwa jina la Green Guard kuanza kufanya mashambulizi dhidi ya
viongozi wa UKAWA kwa sababu tu wameipiku CCM na mawakala wake, katika kujenga
ushawishi kwa wananchi unaotokana na hoja zenye ushahidi wa takwimu za kitafiti
na mtiririko wa mantiki katika kutetea maoni ya wananchi kwenye rasimu ya
katiba.
Kauli hiyo ya Makonda ya kuwaagiza vijana wa Green Guard
wajipange kufanya mashambulizi bila shaka kwa nia ya kuteka, kujeruhi, kutesa
na hata kuua, ambayo imepata baraka za viongozi wakuu wa chama inadhihirsha
kuwa Chama hicho ni
Interahamwe kikundi cha kijeshi kilichokuwa kinatumiwa na
watawala kupambana kwa nguvu na kukandamiza demokrasia na wapinzani wa kisiasa
wa serikali nchini Rwanda hadi kusababisha mauaji ya kimbari nchini humo.
Kauli ya Makonda ambayo Jeshi la Polisi nchini kupitia kwa
msemaji wake, Advera Senzo limesema eti halina taarifa nayo, imedhihirisha kwa
ushahidi kuwa kikundi cha ulinzi cha Green Guard huwa kinatumika kushambulia,
kupiga watu, kuteka, kutesa na hata kuua kama ambavyo kimefanya mara kadhaa
hususan wakati wa chaguzi ndogo.
Aidha Naftal
alimuelezea Makonda wanamfahamu kwa kujulikana kwa umahiri wake wa
kutanguliza tumbo lake na kulinda maslahi ya wakubwa wanaomtumia kwenye makundi
ya ndani ya CCM.
“akiwa Moshi alikokuwa akiwalaghai (na kuwatapeli fedha
akisingizia analipa ada) baadhi ya watu ambao huwa wanamtumia kuwa yuko chuoni
anasoma, wakati hasomi, alikuwa akijulikana mji mzima kwa jinsi ambavyo mtu
yeyote mwenye fedha angeweza kumtumia kwa namna mbalimbali ikiwemo kutoa
matamko hali inayopelekea mara kadhaa kutumika na watu wa nje na ndani ya CCM
kukihujumu chama hicho anachosema yeye ni mwanachama.”alisema
Aliongeza kuwa wakati wa uchaguzi mkuu wa chama hicho mwaka
jana, baada ya kushindwa nafasi aliyokuwa akigombea, Makonda aliandika mambo
mengi akionesha namna ambavyo CCM kinanuka rushwa na kimekubuhu kwa ubakaji wa
demokrasia lakini kitendo cha kupachikwa cheo alichonacho sasa ndani ya
UVCCM kimemfanya ale matapishi yake,na anawaita ni wazalendo.
Alisema pamoja na makelele yake, walau angelikuwa
mwadilifu, bali hana hata chembe ya sifa hiyo na anatembea na lundo la tuhuma
za ufisadi na ubadhirifu, huku mfano mzuri ni kitendo chake cha kula
fedha na kukwamisha uchaguzi wa Vijana wa Chipukizi wa CCM uliokuwa ufanyike
mjini Morogoro.
“Tunaweza kusema mambo mengi kwa namna tunavyomjua, anajua
kuwa hata jina analotumia SI JINA LAKE HALISI, lakini itoshe kusema kuwa tangu
tulipomtangaza Nape Nnauye kuwa ni Vuvuzela namba moja ndani ya CCM na hadi leo
anajulikana hivyo, hatukuwahi kujua kuwa mwingine anayemfuatia kwa ukaribu kwa
uvuvuzela ni Paul Makonda ndio maana watu hawa wako kundi moja.
TAFADHALI ANDIKA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment