Kiingilio
cha chini katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya Taifa ya
Tanzania (Taifa Stars) na Burundi (Intamba Mu Rugamba) itakayochezwa Aprili 26
mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.
Mechi
hiyo itakuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na
Zanzibar, na kiingilio hicho ni kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani.
Kwa wa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C ni sh. 10,000.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari ipo kambini kwenye
hoteli ya Kunduchi Beach kujiandaa kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezeshwa na
waamuzi kutoka nchini Kenya.
Burundi
inatarajia kuwasili nchini keshokutwa (Aprili 22 mwaka huu) tayari kwa ajili ya
mechi hiyo inayotajiwa kuwa ya kusisimua. Mechi hiyo imepangwa kuanza saa 10
jioni.
Wachezaji
wa Taifa Stars waliopo kambini ni Deogratias Munishi, Mwadili Ali, Aidan
Michael, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Hassan Mwasapili, Kelvin Yondani, Said
Moradi, Amri Kiemba, Frank Domayo, Himid Mao, Jonas Mkude, Athanas Mdamu,
Haruna Chanongo, Juma Liuzio, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa, Ramadhan Singano na
Simon Msuva.
Wengine
ni Benedicto Mlekwa, Emma Simwanda, Joram Mgeveje, Omari Kindamba, Edward
Mayunga, Shiraz Sozigwa, Yusuf Mlipili, Said Ally, Abubakar Mohamed, Hashim
Magona, Omari Nyenje, Chunga Zito, Mohammed Saidi, Ayoub Lipati, Abdurahman
Ally na Paul Bundara.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment