Tuesday, March 25, 2014

GAZETI LACHAPISHA SURA YA OBAMA NA MKEWE KUWA NYANI (ONA PICHA)

Gazeti moja nchini Ubelgiji liko katika wakati mgumu baada ya kuchapisha picha ya Rais wa Marekani, Barack Obama na mkewe kuwa ni manyani (Kushoto pichani). Gazeti hilo lenye mlengo wa maendeleo la De Morgen, limelaumiwa kwa ubaguzi wa rangi baada ya kutumia picha na kuandika habari muda mfupi baada ya ziara ya Obama huko Uholanzi jumatatu wiki iliyopita(17/03/2014).

Picha hizo zinaonesha wazi kabisa wawili (Obama na Mkewe) hao kuwa na sura za nyani ikiambatana na chapisho la taariri ya mhariri inayoonesha ubaguzi wa rangi. Kutokana na tukio hilo Mwandishi mwenye asili ya Nigeria, Chika Unigwe aliweka picha ya gazeti hilo katika mtandao wa twitter.

Habari hiyo iliripotiwa kuwa ni tashtiti ambayo pia ilimkebehi Rais Obama kuwa ni muuza bangi. Gazeti hilo lilitoa picha hizo na kuonesha kana kwamba zilitolewa na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, ulieleza mtandao wa Metro jumapili iliyopita.

SOMA ZAIDI . . .

Picha hiyo iliunganishwa na ujumbe uliosomeka “Vladimir Putin ni Rais wa Urusi. Ametutumia picha hizi baada ya kumuomba, na kuamua kutuma picha badala ya maandishi ‘sababu hana muda’ ” gazeti la The Independent lilisema.

Habari hiyo ilizua hisia kubwa miongoni mwa wasomaji, wako baadhi ya wasomaji waliolitetea gazeti hilo, kwa madai kuwa “Ni utani tu”, mmoja wa wasomaji alisema. Mwingine aliandika katika mtandao wa kijamii kwamba “Kwa madai yao, kuna tani na tani ya picha na fulana pia zikimuonesha Bush amechorwa kama nyani”

Hata hivyo kwa kuona makosa yake, gazeti la De Morgen liliomba radhi na kuchapisha radhi hiyo kuhusiana na picha hizo katika toleo lake la jumatatu jana na kukubali kwamba lilifanya makosa kuchapisha picha hizo.

“Ukiangalia kiwango cha mpasuko baada ya chapisho hilo lenye tashtiti yenye kusudio huwezi kuona kama ni utani, bali ni picha inayoonesha ubaguzi wa rangi” gazeti hilo lilisema.

“Tulidhania kimakosa kuwa ubaguzi wa rangi haukubaliki, na kwasababu hiyo basi tulijua litakuwa ni tukio la utani tu”

Uningwe, mwandishi anayeishi Ubelgiji, aliweka picha ya gazeti hilo kwenye mtandao wa twitter kwa kina na kuleta mkanganyiko mkubwa, na kunesha jinsi ambavyo uongo wa jamii ya Wabelgiji zaidi kwenye De Morgen.


No comments:

Post a Comment