Sunday, March 30, 2014

AJALI, AJALI, AJALI YA TATU SIKU YA LEO, BASI LA MANING NICE LAPINDUKA

Ajali zitatumaliza Watanzania, inasikitsha sana kuanzia juzi watu walipoteza maisha ni jumla ya watu 33, mpaka tunakwenda mitamboni jana na leo zimetokea ajali mbili ambapo zote ni barabara ya kuelekea Mtwara.

Nasikitika kukufahamisha kwamba leo tarehe 30-03-2014 majira ya mchana kumetokea ajali nyingine ya basi la Maning Nice namba T643CBB lililokuwa likitokea Dar Es Salaam kuelekea Masasi mkoani Mtwara

Basi hilo lilipinduka lilipokuwa likijaribu kulikwepa Basi la Machinga lililokuwa likitokea Mtwara kwenda Dar Es Salaam. Basi la Machinga lilikuwa liki-overtake malori mawili katika Kijiji cha Mkwajuni, Mkoani Lindi na hivyo kukutana uso kwa uso na Basi la Maning Nice sababu iliyopelekea basi hilo kuacha njia na kupinduka.

hakuna mtu yoyote aliyepoteza maisha, na mpaka sasa hatujajua majeruhi ni wangapi.



No comments:

Post a Comment