Sunday, March 30, 2014

SIMBA, YANGA ZAPIGWA 2 KILA MMOJA, AZAM NA MGAMBO JKT ZASHINDA

Katika mechi ya mzunguko ya Ligi Kuu Bara Simba watoto wa Msimbazi walikuwa wanapambana na wana lambalmba Azam Fc vijana wa Chamanzi. Kipindi cha kwanza kilianza kwa mashambulizi ya kila upande na kupoteza fursa nyingi za kufungana pande zote mbili, lakini mpaka kina isha timu hizo zilikuwa zimefungana goli moja moja.

Katika kipindi cha kwanza dakika ya 16 Hamis Mcha wa Azam aliifungia bao la kwanza timu yake baada ya wachezaji wa timu ya Sima kujichanganya na kuachia mpira miguuni mwa Mcha na kupachika goli safi.



Dakika ya 45 kabla ya kwenda mapumziko Simba walisawaisha goli kupitia mchezaji wake Joseph Owino aliyefunga kwa kichwa baada ya mabeki wa Azam kuzubaa.

Dakika ya 56 Azam Fc wanalambalamba walipata bao la pili kupitia mchezaji wake John Bocco ikiwa ni baada ya Kipre Tchetche kupiga shuti kali ambalo liligonga mwamba na kumkuta Bocco ambauye bila kulaza damu alimalizia kwa kufunga goli.

Mpaka mpiura unakwisha Azam FC 2 Simba 1.

Huko Mpwapwani, Tanga nako Yanga walikuwa wanapambana na Mgambo JKT ambapo Mgambo waliibuka na ushindi wa 2 – 1 dhidi ya mabingwa wa ligi kuu Yanga. Kwa matokeo hayo Azam inazidi kukwea kileleni wakati Yanga wakiendelea kunasa walipofikia na point 46

No comments:

Post a Comment