Sunday, January 05, 2014

PICHA :VIONGOZI MBALIMBALI WASHIRIKI KUAGA MWILI WA WILIAM MGIMWA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakiifariji familia ya marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga na kutoa heshima za mwisho zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilala, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko.  
ANGALIA PICHA ZAIDI...
Mawaziri wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Dkt. William Mgimwa wakati likipakiwa kwenye gari tayari kuanza safari ya kuelekea Uwanja wa ndege kuelekea mkoani Iringa kwa maziko
Mama Maria Nyerere, akitoa heshima za mwisho
Spika wa Bunge Anne Makinda, akitoa heshima za mwisho.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana heshima za mwisho.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, heshima za mwisho.
Baadhi ya Mawaziriki wakiwa katika foleni kuelekea kutoa heshima zao za mwiho.
Mwili ukipakiwa kwenye gari.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakiwa katika shughuli hiyo.

Baadhi ya viongozi wa Serikali waliohudhuria shughuli hiyo.
Baadhi ya Wabunge waliohudhuria shughuli hiyo.


No comments:

Post a Comment