Lindi.
Mahakama ya
Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi,imemuhukumu mkazi wa kijiji cha
Kichangani, kata ya Stesheni, wilayani humo,George Selemani (49) kifungo cha
miaka mitano gerezani,baada ya kupatikana na kosa la wizi wa Ng'ombe mmoja
mwenye thamani ya Sh,900,000/-mali ya Stehen Mallya.
Hukumu hiyo imetolewa
mwishoni mwa wiki iliyopita na Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo,Cosmas
Hemela, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliokuwa umetolewa na upande wa
mashitaka.
Kabla ya kutolewa kwa
hukumu hiyo, mshitakiwa alipewa nafasi ya kujitetea ambapo aliiomba mahakama
imuonelee huruma kwa kumpa adhabu iliyo nafuu,kwani anafamilia inayomtegemea akiwemo
mke na mtoto ambaye kwa sasa anasoma kidato cha nne.ambaye anatakiwa
kumgharimia kimasomo.
Baada ya utetetzi
huo,Hakimu Hemela alimuuliza mwendesha mashitaka mkaguzu wa Polisi, Peter
Komba,kama anakumbukumbu ya makosa ya zamani kwa mshitakiwa na kujibu
mshitakiwa ni mwizi mzoefu, kwani tayari ameshawahi kufungwa zaidi ya mara
mbili kwa makosa ya wizi.
"Mh, Hakimu huyu
mshitakiwa ni mwizi mzoefu kwani tayari ameshawahi kufungwa zaidi ya mara mbili
kutokana na makosa ya aina hii hii ya wizi"Alisema Komba.
Akitoa hukumu kwenye
kesi hiyo namba 40/2012,Hakimu Hemela alisema amesikiliza vilio vya pande zote
mbili,hivyo kutokana na mshitakiwa kuwa ni mwizi mzoefu na kuwahi kufungwa
zaidi ya mara mbili bila ya kujirekebisha, alimuhkumu kifungo cha miaka mitano Jela.
Pia, mahakama hiyo
imeamuru Ng'ombe aliyeibwa kurejeshwa kwa mlalamikaji ,Koplo Stephen Mallya,
ambaye ni askari wa Jeshi la magereza wilayani Nachingwea.
Awali ilidaiwa
mahakamani hapo na mwendesha mashitaka mkaguzi wa Polisi, Peter Komba kuwa mei
07/2012,usiku katika eneo la kijiji cha Chemu Chemu,wilaya ya Nachingwea na mkoa
wa Lindi,mshitakiwa George aliiba Ng'ombe mmoja dume mwenye thamani ya
Sh,900,000/- mali mlalamikaji askari magereza Stephen Mallya.
Komba aliiambia mahakama
hiyo kuwa mshitakiwa alikamatwa na mlalamikaji akisaidiana na wanachi
wengine,akiwa tayari ameshamtoa zizini huku akiwa amemfunga kamba na kuondoka
naye.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment