Idadi ya watu wenye uzito mkubwa katika nchi zinazoendelea
imeongezeka kwa zaidi ya mara tatu toka watu milioni 250 mpaka milioni 904
kwa kipindi cha miaka takriban 30 tokea 1980 mpaka 2008, matokeo hayo ni kwa mujibu wa
taarifa iliyochapishwa na watafiti wa nchini Uingereza.
Wakati huo huo idadi ya watu wenye uzito mkubwa imeongezeka
kwa zaidi ya mara 1.7 kwa nchi zilizoendelea.
Theluthi moja ya watu wazima duniani sawa na watu bilioni
1.46 wana uzito kupita kiasi (au obese), imedai ripoti hiyo ilioandaliwa na taasisi
ya Overseas Development Institute.
Lakini kufikia mwaka 2008watu wengi zaidi walikuwa na uzito
mkubwa na katika nchi zinazoendelea sawa na idadi ya watu milioni 904 kuliko
nchi za kitajiri ambapo ni watu milioni 557.
Sababu za ongezeko kubwa kiasi hicho katika nchi
zinazoendelea tokea mwaka 1980 zinaweza kuwa katika maeneo mawili.
SOMA ZAIDI...
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ni sababu ya kwanza ni vyakula vya
anasa na sababu ya pili ni aina ya maisha watu wanayoishi.
Watu wengi kwenye nchi masikini wanatengeneza kipato cha
kuwatosha kubadilisha mlo toka kwenye vyakula vya nafaka na mboga kwenda kwenye
vyakula vya nyama, mafuta na sukari na kuongezeka kwa maisha ya ubwanyenye.
Kwa sababu hiyo, matokeo ya maisha hayo yamesababisha
ongezeko la maradhi kama saratani, kisukari, magonjwa ya moyo na kupooza.
“Kilichobadilika,” inaeleza ripoti hiyo, “ni kwamba idadi
kubwa ya watu wenye uzito mkubwa ikao katika nchi zinazoendelea, badala ya nchi
zilizoendelea”
No comments:
Post a Comment