Monday, January 27, 2014

DR. LWAITAMA AZUIWA NA SHIRIKA LA NDEGE LA PRECISION

Precision wamdhalilisha Dr. Azaveli Lwaitama(Pichani Kulia) wamshusha kwenye ndege kisa Lugha

Precision wamzalilisha Dr Azaveli Rwaitama mwanza baada ya kumutia polisi ndani ya ndege na kumshitaki kwa kosa la kukataa kutii amri za wahudumu. Kwa sasa anashikiliwa na polisi.

Alikuwa ameketi kwenye kiti cha emergence exit na kuwataka wahudumu wampe maelezo kwa Kiswahili kwani ndege za Precision ni za kitanzania na zinaoparate nchini. Wahudumu walikataa na kumwamuru ahame kama yeye hajui kingereza- Kwa kuanzia hapo polisi waliitwa na kumtia mbaroni.

Ninachojua mimi ni kwamba ndege nyingi hutumia Lugha kuu za kimataifa na Lugha za nchi husika. Ukipanda Ethiopia line au Turkish na zingine nyingi watakupa maelezo kwa Lugha yao ya Taifa na zingine za kimataifa. Inakuwaje leo Tanzania tushindwe kutoa flight instrusctions kwa kiswahili?

Precision mmemkosea Dr Rwaitama mwombeni radhi na mlipeni gharama zote za kusimamisha safari yake ya Bukoba.

No comments:

Post a Comment