Tuesday, December 17, 2013

WALIOKUFA AJALI YA BURDANI WAZIDI KUONGEZEKA

IDADI ya watu waliokufa katika ajali ya basi la Burdani iliyotokea wiki iliyopita, imeongezeka na kufikia 16 baada ya abiria wanne kufariki dunia, imeripotiwa Korogwe.

Basi hilo lilikuwa likitoka Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, kwenda Dar es Salaam na lilipata ajali katika Kijiji cha Taula, Kata ya Kwedizinga, wilayani Handeni, saa moja asubuhi na kuua watu 12.

Akizungumza na Majira jana, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Magunga, wilayani Korogwe, Dkt. Edes John, alisema watu wawili walifariki katika Hospitali ya Bombo wakati wakiendelea kupatiwa matibabu.

Aliwataja watu hao kuwa ni Said Mohamed, mkazi wa Bumbuli wilayani Lushoto na Isack Mbwambo, mkazi wa Korogwe Mjini ambaye ni mtoto wa mwaka mmoja na nusu.

Alisema mmoja alifariki katika Hospitali ya KCMC iliyopo Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro ambaye ni Athuman Said (aliyekuwa kondakta) na Rahma Abdul alifariki katika Hospitali ya Magunga, wote wakazi wa Korogwe.

SOMA ZAIDI...



“Hadi sasa, katika Hospitali ya Magunga wamelazwa wanawake kumi na mwanaume mmoja, KCMC walipelekwa majeruhi 10, Bombo mmoja, waliofariki Hospitali ya Bombo hawakupitia Magunga, walichukuliwa moja kwa moja eneo la ajali.

“Hospitali ya Taifa Muhimbili walipelekwa majeruhi watano akiwemo mdogo wake na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Joel Bendera ambaye ni Francis Bendera,” alisema.

No comments:

Post a Comment