Wednesday, December 18, 2013

TANZANIA NI NCHI YA KIJAMAA, UCHUMI WA SOKO


Tanzania ni nchi ya kijamaa yenye kufuata mfumo wa uchumi wa soko. Hayo yalisemwa leo bungeni wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu na Mipango, Wiliam Lukuvi (Pichani Kushoto) alipokuwa akijibu swali lillloulizwa na Mbunge wa kuteuliwa Mh. James Mbatia.

Mh. Mbatia aliuliza mfumo wa elimu kama bado ni wa ujamaa na kujitegemea kama ilivyokuwa enzi za baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Swali hilo lilielekezwa Wizara ya Elimu ambapo Naibu Waziri, Philipo Mulugo aliomba apewe muda wa kulijibu swali hilo baada ya kutafuta majibu.

Mh. Lukuvi alitoa ufafanuzi huo huku akijibu swali hilo mapema leo (18/12/2013) katika vikao vya bunge vinavyoendelea mjini Dodoma. Mh. Lukuvi aliomba akisema “Mheshimiwa Mwenyekiti naomba kujibu swali aliloulizwa Naibu Waziri wa Elimu na Mh. James Mbatia”


“Tanzania ni nchi ya kijamaa yenye uchumi wa soko unaoambatana na tunu za ujamaa” alisema William Lukuvi


No comments:

Post a Comment