Tuesday, December 17, 2013

MAWAZIRI 4 WAMEKAMATWA

Siku moja baada ya jaribio la mapinduzi kutibuliwa nchini Sudan Kusini, mjumbe maalum wa Marekani nchini humo, Donald Booth,ameambia BBC kuwa maelfu ya watu wametafuta hifadhi katika vituo viwili vya Umoja wa Mataifa mjini Juba.

Bwana Booth amesema kuwa uwanja wa ndege ulifungwa huku huduma za simu zikitatizwa.

Rais Salva Kiir (Pichani Kulia)  amesema kuwa wanajeshi wake walitibua jaribio hilo la mapinduzi huku ripoti zikisema kuwa angalau mawaziri wanne wa zamani wametiwa nguvuni.Mmoja wao Majak D'Agoot ameiambia BBC kwamba hawakutekeleza jaribio la mapinduzi ingawa walikuwa wamemkosoa bwana Kiir katika siku za hivi karibuni.

Mnamo Jumatatu Rais Kiir, anayetoka jamii kubwa ya wa Dink, alilaumu wananajeshi watiifu kwa makamu wa rais wa zamani chini ya serikali ya Kiir Riek Machar kutoka katika kabila dogo la Nuer.

Wasiwasi wa kisiasa umeikumba Sudan Kusini tangu mwezi Julai baada ya bwana Kiir kulivunja baraza lake lote la mawaziri na kuwafuta kazi mawaziri wote akiwemo makamu wake wa Rais bwana Riak Machar.

Kikosi cha kulinda amani cha umoja wa mataifa kimesema kuwa mamia ya raia walikuwa wamekimbilia usalama katika makao yake mjini juba.

TAARIFA HII NI KWA MUJIBU WA BBC SWAHILI


No comments:

Post a Comment