Fainali za kumtafuta ‘Kigoli wa Tanzania’ 2013, zimefikia tamati juzi usiku katika ukumbi wa Letasi Lounge ambapo, Suzan Ndae aliibuka mshindi na kuzawadiwa gari aina ya Noah lenye thamani ya sh. milioni 9.
Fainali hizo zilijumuisha jumla ya washiriki sita ambao walianza kupanda jukwaani kujitambulisha na kufungua shoo kwa kucheza wimbo wa msanii J Martin wa Nigeria kwa pamoja.
Baada ya burudani hiyo bendi ya Malaika ilipanda jukwaani kutumbuiza nyimbo zake mbalimbali baada ya kushuka akapanda msanii Kadija kutoka katika Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT), kabla ya kuwapisha mshiriki mmoja mmoja kupanda tena jukwaani.
Alianza kupanda mshiriki Shuu akifuatiwa na Neema, Brigite, Suzan, Monalisa na kumalizia mshiriki Mariam ambao walicheza wimbo wa Chereko wa msanii wa kizazi kipya nchini, C Pwaa.
Bendi ya muziki wa dansi ya Sky Light nayo pia haikuwa nyuma ilipanda jukwaani kutoa burudani ya washiriki wote kumaliza, ambao waliimba nyimbo zao zikiwemo Karolina pamoja na Mpaka nipate dough.
urudani hiyo ilifuatiwa na nyingine kutoka kwa msanii, Ally Nipishe kutoka THT akiwa na msanii Khadija ambao waliburudisha kabla ya kutajwa Vigoli walioingia tatu bora.
Vigoli walioingia tatu bora walikuwa Suzan, Shuu na Monalisa ambao walipanda jukwaani mmoja mmoja kucheza wimbo wa Sugua gaga na baada ya hapo tatu bora walitajwa ambapo Monalisa alishika nafasi ya tatu, shuu akipata nafasi ya pili huku nafasi ya kwanza akishika Suzan.
Baada ya kutangazwa mshindi na kukabidhiwa funguo za gari, Suzan ambaye aliwahi kushiriki shindano la Miss Tabata na kushinda taji la Talent, alisema atalitumia gari hilo kwa mafanikio.
"Shindano lilikuwa gumu kwangu, ila nashukuru nimeweza kufanikiwa kupata ushindi wa gari na ninawashukuru wote waliofanikisha niweze kushinda na ninaahidi nitatumia vizuri kipaji changu," alisema Suzan.
No comments:
Post a Comment