Monday, December 23, 2013

MAJANGA: AISHI PAMOJA NA MUMEWE NA NYUMBA NDOGO

Mwanamke mmoja anayeishi na wanaume wawili ametoka na ufumbuzi wa ajabu…aliweza kuwaamishia wote kwenye nyumba moja, na yeye kuishi nao.
Maria Vogel, 33, mzaliwa wa Bulawayo, sasa hivi anaishi na wanaume wawili huko Uingereza, Barking, London akiwa pia na watoto wake Laura (16) na Amy (12). Wanaume anaoishi nao ni Paul Butzki na Peter Gruman.
PICHA KULIA: Maria akiwa na Paul na Peter na watoto wake Laura na Amy

Maria ambaye amekulia Saurcetown na kusoma shule Northlea, alikuwa na miaka 15 alipokutana na Paul akiwa shule na kupata ujauzito miaka miwili baadae na ndipo alipozaliwa Laura.
Wawili hao wakafunga ndoa kabla mtoto wao wa pili Amy hajazaliwa, lakini mahusiano yao yaligonga mwamba 2006.
PICHA KUSHOTO: Maria akiwa na Paul na Peter (Kulia)

Maria aliliambia gazeti la Daily Mirror:”Paul hakuwa na kazi kwa zaidi ya miezi sita, na hiyo ilileta shida sana kwenye mahusiano yetu. Msongo wa mawazo ukasababisha kupungua kufanya mapenzi”
“Pamoja na kwamba tuliendelea kuwa pamoja, tuliendelea kuishi kama kawaida pamoja na kwamba tulipoteza hamu ya mapenzi, mahusiano yalikuwa ni kaka na dada zaidi kuliko wapenzi”
Wakati huo huo meneja mpya, Peter, alianza kazi kazini kwa Maria.

“nikafahamishwa kwa Peter na tuliposalimiana tu nikahisi kuna mvuto kwa kiasi kikubwa” alisema Maria
“Mpaka kufikia hapo nilikuwa na furaha ya ndoa na mahusiano ya miaka 13 na mume wangu mpenzi na sikuwahi kufikiria kuwa na mwanaume mwingine”
Peter ambaye alikuwa na mke wakati huo, anakumbuka jinsi alivyovutiwa na Maria, “ilikuwa ni upendo wa ghafla” Alisema Peter.
Peter na Maria walianza kukutana kisiri siri, “tulikutana bar mchana” alisema Maria. Sikumoja akanishika mguuni, mwili mzima ukastuka kwa hisia. Nilijua sio sahihi lakini muda si mrefu tukaanza kufanya mapenzi”
Mahusiano yao yaliendelea kwa zaidi ya mwaka kabla Paul hajanasa meseji kwenye simu ya Maria. Lakini Maria alifanikiwa kumshawishi Paul kuwa wao ni marafiki tu na si zaidi.
Miezi michache baadaye mpenzi wake aliachana na mkewe na kuhamia Beds toka Luton ili awe karibu na Maria anaye ishi Barking.
“nilizidi kuvutiwa na Peter” alisema Maria. “Paul aliposafiri kikazi ni Peter ndo alikuwa anawapeleka watoto shoping na kwanunulia vizawadi mbalimbali”
lakini siku ya wapendanao (Valentine’s Day) ya 2010, Maria anadai alishindwa kuficha. “Nilianza kuhisi kuwa ntakuwa na Peter kwenye maisha yangu,” alisema. Hiyvo nikafunguka kwa Paul, na kuondoka nyumbani kuhamia kwa Peter”
Paul na watoto wakachanganyikiwa. “nilishtuka na nilivunjika moyo. Sikuamini Maria ameniacha” alisema Paul.
Miezi michache iliyofuata walipangiana jinsi ya kulea watoto. “Nilijiskia vibaya kuibomoa familia yangu, hivyo baada ya kazi nilikwenda kusafisha na kumpikia Paul na watoto alafu narudi nyumbani kwa Peter” alisema Maria.

Wanaume hao walianza kuwa marafiki mwaka jana, Maria alichoka kwenda na kurudi kwa mumewe na kwa mpenzi wake.
Hiyvo akatoka na ufumbuzi wa zoezi hilo, na kuamua kumuamishia Peter kwenye familia yake nyumbani kwa Paul.
“Watu wanaweza kuona ni ajabu lakini nawapenda wanaume wangu na sikuweza kuchagua kati yao” alisema Maria.

“nilipoachana na Paul nilijiskia kama kuna tundu kubwa kwenye maisha yangu, lakini pia nikifikiria kutomuona Peter muyo unavunjika. Kwa hiyo kuishi nao ndio njia pekee”


No comments:

Post a Comment