Kampuni ya simu za mkononi nchini
Vodacom imekabidhi msaada wa kompyuta 3 zenye thamani ya shilingi Milioni 5.3 katika
klabu ya Waandishi wa Habari (CPC) mkoani hapa.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi wa wanahabari hao Ofisa mahusiano wa kampuni hiyo Salum Mwalimu alisema kuwa msaada huo ni kwa ajili ya kuwarahisishia waandishi wa habari mkoani hapa utendaji wa kazi zao.
“Kwa kutambua mchango mkubwa unaofanywa na waandishi wa habari pamoja na vyombo vya habari katika kutimiza majukumu yetu ya kila siku tumeona ni vema kuwawezesha waandishi wa habari vitendea kazi ili kuwarahishia kazi zao.” Alisema Mwalimu.
Naye Katibu wa CPC Israel Mgussi aliishukuru kampuni ya Vodacom kwa msaada huo kwani ilikuwa ni ahadi yao ya muda mrefu kwa klabu tangu Februali mwaka huu na kusema kuwa kupitia mashine hizo wanahabari mkoani hapa wataweza kuzitumia katika kuandika habari zao kwa urahisi pamoja na kuingiza pato katika klabu hiyo.
Kwa upande wake mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Fatma Ally aliitaka kampuni hiyo kuboresha mahusiano mazuri na waandishi wa habari nchini katika utendaji wao wa kazi zakila siku ili waweze kufanikiwa katika biashara zao.
Aidha aliongeza kwa waandishi wa habari mkoani hapa kutumia vifaa hivyo katika kuandika habari zenye uhakika katika kuelimisha jamii pamoja na kutumia fulsa zinazo jitokeza kujiinua kimaisha ikiwa ni pamoja na kuwa wajasiliamali katika ufugaji nyuki, kilimo cha biashara na shughuli nyingine kwakuwa wao ni kiungo muhimu kwa jamii.

No comments:
Post a Comment