Thursday, December 05, 2013

JELA MIAKA 10 KWA KUBAKA MBUZI


Katana Kitsao Gona (28) (Pichani) toka Malindi, Kenya alihukumiwa kwenda jela miaka 10 baada ya kukiri kosa la kumbaka mbuzi.

Kijana huyo alikutwa na hatia ya kumbaka mbuzi huyo mwenye jinsia ya kike na kuhukumiwa jela kwa kitendo hicho cha ajabu na mahakama ya Malindi nchini Kenya.

katika mahakama hiyo mbuzi huyo pia alikuwepo wakati Katana Gona akihukumiwa adhabu hiyo ambayo ataanza kuitumikia mara moja baada ya kutolewa.

Katana alikutwa na mpita njia akiwa uchi huku anambaka mbuzi huyo mnamo tarehe 25 mwezi november 2013 huku mbuzi huyo akiwa amefungwa kamba, liliandika gazeti la The Star la nchini Kenya.

Taarifa zilimfikia moja kwa moja mmiliki wa mbuzi huyo ambaye alikuja na kundi kubwa la watu na kumkuta live Katana akifanya mambo.


hata hivyo Katana baada ya kukiri kosa hilo aliomba radhi mahakamani na kudai kuwa hakuwa na jinsi kwani mkewe ambaye anamtegemea ni mlemavu.

Hata hivyo Katana amepewa fursa ya kukata rufaa ndani ya siku 14.

No comments:

Post a Comment