Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), limeanza kutoa mgawo wa tiketi Fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil ambapo Tanzania imepatiwa tiketi 260.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwenye vyombo vya habari na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura ilieleza kuwa Watanzania wanaohitaji tiketi hizo wanatakiwa kutuma maombi.
Wambura alisema hakuna tiketi zitakazoombwa FIFA, bila kuwepo maombi kwa maandishi hivyo Watanzania wanatakiwa watume maombi TFF kwa maandishi wakielezea aina ya tiketi na mechi wanazohitaji kwenda kushuhudia.
Wambura alisema tiketi zilizopo kwa Tanzania ni za hatua ya makundi (ukiondoa mechi ya ufunguzi), raundi ya 16 bora, robo fainali na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu ni dola 250.
Pia alisema kwa mechi za ufunguzi, nusu fainali mbili na fainali ambazo ni mechi namba 1, 61, 52 na 64 ni tiketi kumi tu ndizo zitakazopatikana ambazo bei zake zitakuwa kwa viwango vitatu tofauti.
Wambura alisema mechi ya ufunguzi tiketi zake ni dola za Marekani 495, 330 na 220. Hatua ya makundi (mechi namba 2-48) ni dola 175, 135 na 90. Hatua ya 16 bora (mechi namba 49-56) ni dola 220, 165 na 110.
Alisema robo fainali ambayo itakuwa mechi namba 57-60 ni dola 330, 220 na 165 wakati nusu fainali ambayo ni mechi namba 61 na 62 ni dola 660, 440 na 275 huku mechi ya mshindi wa tatu ni dola 330, 220 na 165. Kiingilio kwa fainali kitakuwa dola 990, 660 na 440.
“FIFA watatoa tiketi kwa Watanzania ambao wataleta maombi yao TFF kwa maandishi hivyo tunasisitiza maombi ya tiketi yatakayofanyiwa kazi ni yale ambayo yamewasilishwa kwa maandishi,” alisema.

No comments:
Post a Comment