Operesheni Tokomeza Majangili ilitekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya Balozi Khamis Kagasheki, ikishirikiana wa Wizara ya Mambo ya Ndani chini ya Emmanuel Nchimbi, Wizara ya Ulinzi ikiwa chini ya Shamsi Nahodha Vuai na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikiongozwa na Mathayo David Mathayo.
Aidha Rais amelitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania liunde tume itakayo chunguza na kuwawajibisha kwa mujibu wa sharia wale
wote waliojihusisha na uhalifuhuo.
Kabla ya tukio hilo Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki alitangaza Bungeni kuwa amejiuzulu kutoka katika wadhifa wake huo kutokana na Ripoti ya Kamati hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali na Raisi, Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda alidai kuwa kuondolewa kwa mawaziri hao kumeridhiwa na Rais kutokana na ripoti hiyo.
Alisema pia kutokana na taarifa ya ripoti hiyo, Rais ameona umuhimu wa mawaziri hao kutoka katika wizara hizo kutengua nyadhifa zao.
Alidai kuwa operesheni tokomeza majangili ilikwa na nia njema ingawa utendaji wake na namna ilivyosimamiwa ndio imepoteza maana.
No comments:
Post a Comment