Friday, November 08, 2013

PAPA FRANCIS ASHTUA UMATI WA WATU




PAPA FRANCIS ASHANGAZA WENGI…

 * AGUSA NYOYO ZA WATU...


Bado kuna watu hawamkubali Papa Francis na mitazamo yake. Mfano wa mitazamo hiyo ni kuwa Papa wa kwanza kutamka hadhatani kuwa mashoga wanaweza kwenda mbinguni.

Mfano mwingine ni pale alipoamua kuondoa kinga za risasi zinazolizunguka gari lake ili tu awe karibu zaidi na waumini pamoja na wakristo wenzake.

Papa Francis anachojali ni kuwaombea watu na kuombeana, lakini pia amewashangaza wengi wiki hii wakati anatoka katika makao makuu yake ya St.Peter alipokuwa kwenye gari lake la wazi(PICHANI JUU) na kumuona mtu ambaye alikuwa na sura ya ajabu kwenye kundi la watu.

Papa Francis aliamua kufanya jambo ambalo halifikiriki, alimsogelea mtu huyo ambaye amejawa na mapunye na kumkumbatia (CHINI KULIA) na kisha kumbusu(PICHA YA KATI) katika paji la uso.

Tofauti na wengi wetu, kiongozi huyo wa kanisa Katoliki hakuogopa kumsogelea mtu huyo mgonjwa. Lakini alimshika na kumbusu kwenye tama kisha akamuombea.

Ujasiri na kujituma sio tu kujilinda, bali ni kufanya jambo ili kufikia mahitaji ya watu…na Papa Francis analifahamu hilo.


No comments:

Post a Comment