Friday, November 08, 2013

DHL YASHTAKIWA KWA KUFUKUZA KAZI WAISLAM

Kundi la waislamu walioajiriwa katika kampuni ya kusafirisha vifurushi ya DHL wamefungua kesi ya malalamiko wakidai haki sawa kwa wafanyakazi huku wakilalamikia kampuni hiyo kuwafukuza kazi kwa sababu ya kuswali.

Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la Times la Marekani, Mohamed Maow, 27, mkimbizi kutoka nchini Somalia ambaye amefanya kazi DHL, Hebron, Kentucky nchini Marekani, alidai mwanzo kampuni hiyo ilikubali ombi la waisalamu kuswali wakati wa mapumziko mara tano kwa siku ikiwa ni moja ya nguzo za dini ya kiislamu

‘Wametufukuza kazi’, Maow alidai kuwa DHL ilibadilisha taratibu kama ambavyo iliripotiwa katika jarida la Cincinnati.

Maow ni mmoja kati ya wafanyakazi 11 wanaoilalamikia DHL na waislam wengine 13 wanatarajiwa kuungana nao. Baraza la Waislam jimbo la Ohio la mahusiano ya Waislamu Wamarekani imefungua malalamiko hayo kwa niaba yao.

DHL haikujibu lolote walipoulizwa kuhusu ripoti hiyo ya jarida la Cincnnati.





No comments:

Post a Comment