Friday, October 18, 2013

GOSBY APATA SHAVU


MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini mkali wa 'King of Swaghili' Gosbert Kibanza 'Gosby' amekuwa msanii wa kwanza Afrika Mashariki kuingiza nyimbo yake katika mixtape ya Coast to Coast nchini Marekani.

Nyimbo ya msanii huyo  iliyoingia katika mixtape inajulikana kwa jina la BMS 'Baby Making Swag', ambapo msanii huyo aliweza kupokea email mwanzoni mwa wiki hii  iliyothibitisha kuingia kwa nyimbo hiyo.


Akizungumza na jarida hili kwa njia ya simu Gosby aliweka wazi kuwa amekuwa miongoni wa wasanii wanaotafuta nafasi za kuutangaza muziki nje ya nchi.

Aliweka wazi kuwa kilichomsaidia yeye ni kutafuta nafasi na kutumia mitandao mbalimbali ya kijamii ili aweze kuutangaza muziki wake ingawa pia ubora wa muziki, uliojaa ubunifu na kuchanganya lugha ya kiswahili na kingereza ndio kilichomsaidia nyimbo hiyo kuchaguliwa.

"Jamaa wa Coast to Coast waliiona nyimbo yangu kwenye mtandao mmoja wa nchini Marekani unaoitwa 'Rapgenius' ambayo huweka mashairi ya wasanii wa muziki wakubwa wa Marekani na duniani kwa sababu mimi ni msanii wa pekee Afrika Mashariki hivyo wao ilikuwa rahisi kunipa" alisema Gosby na kuongezea kuwa.

" Baada ya kunipata waliomba niweke nyimbo yangu hii ya BMS ili watu waipigie kura hali iliyopelekea nyimbo yangu kufanikiwa kuingia kwenye mixtape" alisema.

Pamoja na hayo msanii huyo hivi karibuni ameachia nyimbo inayojulikana kwa jina la 'Monifere' aliowashirikisha baadhi ya wasanii wa hapa nchini akiwemo Vanessa Mdee.





No comments:

Post a Comment