Monday, October 21, 2013

KANYE WEST ATOA KASHFA



RAPPER kutoka nchini Marekani, Kanye West ameonesha kitendo ambacho kimetafsiriwa kama kumkosea mungu baada ya kuimba wimbo unaojulikana kwa jina la 'Jesus Walk' ambayo ipo kwenye albamu ya 'College Dropout'.

Kitendo hicho ambacho kimetafsiriwa na baadhi ya mashabiki wake waliohudhuria shoo yake hivi karibuni baada ya rapper huyo kuimba nyimbo hiyo ambapo alitokea mtu aliyevaa nguo kama Yesu.Rapper huyo ambaye alikuwa na msaidizi wake wa kike kwenye kuimba waliinama mbele ya mtu huyo kwa kuonesha ishara ya kuabudu na baadaye wakaanza kuimba wimbo huo.

Kitendo hiko cha kumuweka mtu aliyefanana na Yesu ambaye amevalia mavazi hayo ndicho kilichotafsiriwa na baadhi ya mashabiki wake.



No comments:

Post a Comment